FURSA 10 ZA BIASHARA


Inaandikwa na Alex Mr motivation

Baada ya kupata maneno muhimu na elimu nyingi za motivation, sasa leo tuliangalie biashara kumi unazoweza kuanza mwaka huu 2019 kwa mafanikio makubwa.

1.Bidhaa za chakula.
Kwa kuwa watu bado wanakula, na wataendelea kula siku zijazo, kuanza biashara ya kuuza bidhaa za chakula ni hatua sahihi kwako kuchukua. Hapa unaweza kuuza na kusambaza bidhaa za chakula kama nafaka, mafuta na bidhaa nyingine muhimu.Angalia uhitaji wa bidhaa za vyakula kwa wale wanaokuzunguka au unaoweza kuwafikia kisha wapatie bidhaa hizo kwa kiwango na gharama ambazo wanaweza kumudu huku wewe ukipata faidia ili biashara iweze kuendelea.Uzuri wa biashara ya bidhaa za chakula unaweza kuanza na mtaji kidogo, ukatafutabidhaa zilizo bora na kuweza kuwasambazia watu kule walipo.Biashara ya mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine zina uhitaji mkubwa kwa watu.

2 .Huduma za chakula
Biashara nyingine unayoweza kuanza kwa mafanikio mwaka huu 2018 ni biashara ya utoaji wa huduma za chakula. Hapa unatengeneza na kuuza chakula bora ambacho watu wanaweza kukimudu.Uzuri wa biashara hii ni kwamba, watu wengi wanabanwa na kazi au biashara zao na hivyo hawawezi kuandaa vyakula vyao, hasa vya mchana. Hivyo kwa kuwajua watuwa aina hii na namna unavyoweza kuwafikia, unaweza kuwapatia chakula ambacho ni bora kwa gharama wanazoweza kulipia.Kingine muhimu ni kwamba watu kwa sasawanajali sana afya zao, hivyo wanakula mlo bora, unaweza kutumia nafasi hii kutoavyakula bora kiafya badala ya vyakula vya haraka ambavyo siyo bora.Unaweza pia kutoa huduma ya matunda, juisi na huduma nyingine za chakula kwa wale wenye uhitaji.


3.Bidhaa za mavazi.
Kama ambavyo tumeona, watu wanaendelea kuvaa nguo, bila ya kujali mambo ni magumu au la. Hivyo unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa bidhaaza mavazi. Hapa unauza mavazi kama nguo, viatu na mengineyo.Unachohitaji hapa ni kujua uhitaji wa watu kwa wakati mbalimbali. Kwa mfano kipindi cha mwanzo wa mwaka bidhaa nyingi za mavazi zinazotoka ni zile zinazohusiana namavazi ya shule. Pia katika kipindi cha sikukuu, watu wanajibana wawezavyo ili wavae nguo mpya.Unapochagua kuingia kwenye biashara hii ya bidhaa za mavazi, angalia aina ya watu ambao ni wanunuaji wazuri. Mfano mavazi ya wanawake na watoto yanatoka zaidi kibiashara kuliko mavazi ya aina nyingine.Uzuri wa biashara ya bidhaa za mavazi ni kwamba, unaweza kuianza kwa hatua ndogo sana, huhitaji hata kuwa na eneo la biashara. Unaweza kuchagua wateja unaowalenga, ukachagua bidhaa zao kisha kuwasambazia au kuwatangazia kwa njia ya mtandao.

4.Biashara ya huduma za mavazi.
Huduma za mavazi ni aina nyingine ya biashara unayoweza kuanza, ambayo itakuwezesha kupiga hatua kubwa. Kama una ubunifu wa mavazi, au unaona uhitaji wa mavazi ya aina fulani, unaweza kutoa huduma ya kuandaa mavazi hayo.Hapa tunazungumzia kutoa huduma ya kuwaandalia watu mavazi kwa namna wanavyoyataka. Pia kuwasaidia watu kurekebisha mavazi yao. Biashara hii unaweza kuifanya kama unao ufundi wa kutengeneza mavazi. Lakini hata kama huna, unaweza kupata mtu mwenye ufundi ukawa unampa maelekezo na wewe kuwa na kazi ya kutafuta masoko au kusambaza yale mavazi yanayotengenezwa.Siku hizi zipo mashine ambazo ni rahisi kutumia kushona mavazi ya aina mbalimbali ambazo unaweza kuwa nazo na kuanza kiwanda chako kidogo cha mavazi.


5.Ufugaji wa kibiashara – kuku.
Hakuna familia ya asili ya kiafrika ambayo haijawahi kufuga kuku. Na kuku ni moja ya wanyama ambao soko lake halijawahi kuyumba. Zimekuja biashara za ndege wa aina mbalimbali kama kware lakini zimepita na kuacha biashara ya kuku ikiwa imara. Huhitaji kumshawishi mtu kwamba anahitaji kula nyama ya kuku, au kula mayai, ni kitu ambacho kwa wengine ni ufahari.Unaweza kuingia kwenye ufugaji wa kibiashara na kufuga kuku ambao utaweza kuuza mayai, kuuza vifaranga na hata kuuza kuku wenyewe. Unaweza kufuga kuku wa kienyeji, kuku chotara na hata kuku wa kisasa kabisa. Unachohitaji kuangalia ni uwezo wako na uhitaji wa soko unalolenga.Uzuri wa ufugaji wa kuku ni kitu unaweza kuanza kwa hatua ndogo na kukuza. Pia unaweza kufanya huku ukiendelea kufanyavitu vingine. Pia itakuhitaji uwe makini ili ufugaji wako ukue.


6.Ufugaji kibiashara – samaki.
Samaki ni chakula kingine ambacho kina uhitaji mkubwa sana kwenye jamii zetu. Nimboga ambayo ina uhitaji mkubwa na hivyo ukiweza kuzalisha kwa kiwango kizuri, ni biashara nzuri kwako kufanya.Ufugaji wa samaki kwa sasa umerahisishwa kutokana na upatikanaji wahuduma muhimu za samaki. Huduma kama vyakula vya samaki, ujenzi bora wa mabwawa ya kufugia samaki zimefanya ufugaji wa kibiashara wa samaki kuwezekana.Japo ufugaji wa samaki unahitaji mtaji mkubwa, inawezekana pia kuanza kidogo na ukafanya vizuri.

7.Kilimo biashara – mbogamboga na matunda ya muda mfupi.
Hata kama uchumi ni mgumu kiasi gani, watu hawatakula chakula bila ya kitunguu, bila ya nyanya, bila ya bamia. Watu wataendelea kula mchicha, matembele na mboga nyingine. Na muhimu zaidi matunda kama matango, matikiti maji na hata ndizi ni vyakula ambavyo kila mtu ana uhitaji navyo.Hivyo eneo unaloweza kuingia kibiashara mwaka 2018 kulingana na nafasi na uwezowako ni kilimo biashara cha mbogamboga na matunda ya muda mfupi. Ninaposema kilimo biashara namaanisha ulime kwa lengo la kuuza, hivyo kulima kwa viwango vizuri na ubora ambao unakubalika na sokounalolenga.Unaweza kulenga wanunuaji wa rejareja aukuuza kwa wanaonunua jumla, kama mahoteli au maduka makubwa.

8.Kilimo biashara – mazao ya chakula.
Mazao ya chakula kama nafaka, mahindi, maharagwe na mpunga ndiyo mazao yanayoongoza kwa kuliwa sana kwenye jamii zetu. Hivyo hili ni eneo ambalo unaweza kuingia kibiashara na ukafanya vizuri kwa mwaka huu 2018. Unaweza kuingia kwenye kilimo moja kwa moja na ukalima kibiashara, kwa njia ambayo utazalisha kwa kiwango kikubwa na kwa ubora wa kuweza kuuza.Lakini pia kama huwezi kulima, kwa kukosa nafasi au usimamizi mzuri, unaweza kununua mazao hayo kwa wingi kwenye msimu wa mavuno, kuyaongeza thamani na kuyauza kwa wahitaji. Mfano kununua mpunga wakati wa mavuno, kuukoboa, kuuhifadhi kwenye vifungashio vizuri na kuuza kwa watumiaji ni biashara ambayo inaweza kukupeleka kwenye mafanikio makubwa 2018.

9.Biashara ya vyakula vya mifugo na huduma zake.
Watu sasa wanafuga, kuanzia kuku, mbuzi, ng’ombe, sungura, samaki na kadhalika. Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa huduma mbalimbali za kuwezesha wafugaji kupata mafanikio kwenye ufugaji wao.Hapa unaweza kuingia kwenye biashara yakuuza vyakula vya mifugo, kuuza madawa na virutubisho vya mifugo na hata kutoa huduma za vyakula mbadala kwa wafugaji.Na kama wewe ni mfugaji au una utaalamukuhusu mifugo, unaweza kutoa ushauri kwa wafugaji kibiashara pia.

10.Huduma za ushauri wa kitaalamu.
Kwa jambo lolote ambalo umesomea, au umeshakuwa na uzoefu nalo, kuna watu ambao wamekwama na hawajui wafanye nini. Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa lile eneo ambalo una utaalamu au uzoefu nalo.Kama umesomea mambo ya afya unawezakutoa ushauri wa kiafya kwa watu na wakakulipa. Kama umesomea au una uzoefu kwenye biashara, unaweza kuwashauri watu kuhusu biashara na wakakulipa.Angalia kipi unajua na watu hawajui, kisha wape ushauri kwa njia ambayo watakulipa.Nyongeza; uza taarifa na maarifa kwa njia ya mtandao wa intaneti.Tunaishi kwenye zama za kipekee sana, zama ambazo kila mtu anaweza kuzalisha chochote anachoweza kuzalisha bila ya kuziwa na yeyote, kama tu havunji sheria.Hivyo kama kuna vitu unafahamu, kupitia uzoefu, kujifunza au kutafiti, ambavyo vinaweza kuwasaidia watu, unaweza kuweka kwenye njia ambayo watu wanaweza kununua.Unaweza kuweka kwenye mfumo wa kitabu na kuwauzia watu, unaweza kuandaa kwa mfumo wa semina au kozi ambayo watu wanajiandikisha na kusoma.Uzuri ni kwamba, yote hayo unaweza kuyafanya bila hata ya kuwa na eneo la biashara, bila hata ya kuweka shilingi mia. Unachohitaji ni kutumia vizuri mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuwafikia wale wenye uhitaji na kuwapa taarifa na maarifa yanayoweza kuwasaidia.Hizo ndizo biashara kumi, na nyongeza unazoweza kufanya mwaka huu 2018 na ukaweza kupiga hatua kubwa kwenye mafanikio.Muhimu; katika makala hii, nimegusia kwa juu kuhusu kila biashara niliyotaja, kabla hujaingia kwenye biashara yoyote kati ya hizo, na hata nyingine yoyote, fanya utafiti wako, jifunze kuhusu biashara hiyo, ongea na wanaofanya biashara hiyo, ongea na wenye uhitaji wa biashara hiyo, kisha jua unaingiaje ili kutoa thamani zaidi.Muhimu zaidi; asikudanganye mtu yeyote kwamba ipo biashara ya mkato na ya haraka ya kufanikiwa, kila biashara itakuhitaji uweke juhudi kubwa, uwe mvumilivu na uweke muda ili kufanikiwa. Hivyo unapochagua kuingia kwenye biashara yoyote, ingia ukijua hilo, itakusaidia kupambana.


DILEX BUSINESS SOLUTION
Kama una wazo la kufanya biashara hapa Tanzania na ungependa kumiliki kampuni yako au jina la biashara lako,* huduma yetu ni kukusaidia kufaniki
sha usajiri wa biashara yako. Tutumie message yenye neno “KAMPUNI” Whatsapp namnba 0716762015 kupata maelezo zaidi juu ya huduma yetu.

OFISI ZETU
Tunapatikana, Mwalimu.J.K.Nyerere Trade Fair ground(SABA SABA), PLOT No.436, BLOCK A, Kilwa Road, Dar es salaam, Tanzania

Thanks
Contact us DILEX BUSINESS SOLUTION
FACEBOOK PAGE: Dilex business solution
Tell phone No: 0716762015
WHATSAPP :0716762015
E-MAIL: info@dilex.co.tz
Instagram: Dilex business solution

2 comments

  1. nsurii company

    thanx dilex

  2. nsurii company

    Pia kupata maarifa zaidi namna ya kuondokana na umazkini tmbelea blog hii nsurii.blogspot.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *