MIFUMO YA UENDESHAJI BIASHARA TANZANIA


UNAWEZAJE KUCHAGUA MFUMO GANI UTUMIE KUFANYA BIASHARA (KAMPUNI AU JINA LA BIASHARA)- ZIJUE FAIDA NA HASARA ZAKE.

Inaandikwa na Engineer Mr Motivation

Habari ndugu zangu, kiukweli kuna mifumo tofauti tofauti ambayo unaweza kutumia kufanya biashara, na kila mfumo wa uendeshaji wa biashara una faida yake na hasara zake, Fuatilia maelezo ya kila mfumo ukitilia maanani faida na hasara za kila mfumo, Unaweza pia sisi DILEX BUSINESS SOLUTION kwa ajili ya Ushauri wa masuala ya biashara kukushauri kulingana na mazingira yako utakayofanyia biashara.
Hasa unatakiwa kujua zaidi mambo ya kisheria katika mfumo utakaoamua kuutumia kuendehsa baishara yako ili isije ikakuletea shida huko mbeleni, maamuzi ya mfumo upi uuchukue inategemea zaidi sheria za ndani ya nchi husika, pia inategemea ukubwa wa mtaji wako nk.


1. NAMBA MOJA
Mtu mmoja (sole proprietor)
Hii ni biashara inayoendeshwa na mtu mmoja tu kwa kutumia jina lake binafsi au kusajili brela jina la biashara tofauti na jina lake binafsi

Faida yake kuanzisha ni rahisi
-Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu

Hasara yake
-Biashara ikipata shida mmiliki anahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
-Yaani biashara ikidaiwa mali za mmiliki kama nyumba, gari, shamba zitauzwa ili kulipa madeni.

2. NAMBA MBILI
Ushirika au Partnership (watu wawili kwenda juu)
Hii ni biashara inayoendeshwa na watu wawili au zaidi kwa mfumo ule ule wa mtu mmoja lakini hapa ni lazima kusajili jina la biashara brela na kuandika mkataba wa ushirika yaani Partnership Agreement

Faida yake
-Kuanzisha ni rahisi
-Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu japo sio kama biashara ya mtu mmoja

Hasara yake
-Biashara ikipata shida wamiliki wanahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
-Yaani biashara ikidaiwa mali za wamiliki kama nyumba, gari, shamba zitauzwa ili kulipa madeni
-Mikataba inayoingiwa na mmoja wa washirika huwabana na wengine wasiohusika

3. NAMBA TATU
Kampuni ya umma (public companies)(zaidi ya watu wawili bila ukomo)
Kampuni za uma ni zile zinazoitwa kwa kiingereza Public Limited Companies by Share au kwa kifupi PLC. Hizi kampuni zinakuwa na wanahisa bila ukomo na hisa zake huwa zinauzwa kwenye masoko ya hisa kwa uwazi bila siri. Biashara zake husimamiwa na utawala ambao mkurugenzi wake huchaguliwa na bodi ya wakurugenzi ambao hasa ndio wamiliki wa kampuni kwa niaba ya wana hisa wote.

Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
-Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
-Ni rahisi kuvutia mitaji mikubwa kupitia masoko ya hisa

Hasara yake
-Haina usiri hivyo ni hatari kwani washindani wa biashara husika wanaweza kutumia taarifa hizo kujipanga
-Rasilimali muda na pesa kupotea kwa shughuli za ndefu za kihasibu, kisheria na za kodi za serikali. Kwa ufupi paper work ni kubwa, inafuatiliwa sana na TRA, BRELA na taasisi mbalimbali za udhibiti na uhakiki.


4. NAMBA NNE
Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa hisa
Kampuni za binafsi ni zile zinazoitwa kwa kiingereza Private Limited Companies by Share. Hizi kampuni zinakuwa na wanahisa kuanzia wawili mpaka 50 na hisa zake haziruhusiwi kuuzwa kwenye masoko ya hisa au kwa uwazi wa aina yeyote. Biashara zake husimamiwa na utawala ambao mkurugenzi wake huchaguliwa na bodi ya wakurugenzi ambao hasa ndio wamiliki wa kampuni kwa niaba ya wana hisa wote.

Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
-Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
-Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
-Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma

Hasara yake
-Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
-Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
-Kampuni hii ni lazima angalau iwe na wakurugenzi 2, katibu na
Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

5. NAMBA TANO-ILA HII SASA HIVI ZIMEFUTWA NA HAZISAJILIWI TENA KAMA KAMPUNI
Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa udhamini
(private companies limited by guarantees) (watu wawili hadi 50)
Kampuni hizi hufanana na zile za binafsi isipokuwa kampuni binafsi zenye ukomo wa udhamini huwa ni kampuni zisizo za faida na kwa hiyo wadhamini wake hawaruhusiwi kugawana faida. Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali hasa yale ya uwanaharakati zinaanzishwa kwa kutumia mfumo huu badala ya ule wa NGO au CBO kwa sababu za usalama wa kisheria. Mashirika yalisajiliwa kama kampuni yenye ukomo wa wa udhamini zinalindwa na sheria za usajili wa makampuni ambayo wanasiasa hawawezi kufuta kampuni hata kama inaendesha harakati zinazoichukiza serikali.

Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
-Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio kwa wadhamini
-Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
-Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma

Hasara yake
-Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
-Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
-Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

6. NAMBA SITA
Jumuiya (association)
Jumuiya ni muungano wa watu au taasisi zenye lengo moja lizilo la kiserikali au kibiashara
Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
-Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake
-Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
-Ugomvi wa mara kwa mara
-Haina kinga kwa waazilishi ukilinganisha na makampuni

7. NAMBA SABA
Vyama vya ushirika Vyama vya ushirika ni muunganiko wa aidha wafanyakazi au wakulima kwa lengo la kukuza umiliki katika maeneo yao ya kazi au masoko ya biashara
Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
-Inavutia wahisani
-Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake
-Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
-Haina kinga kwa waazilishi ukilinganisha na makampuni.

8. NAMBA NANE
Mashirika yasiyo ya kiserikali Bodi ya wadhamini (Board of Trustee)
Faida yake
-Utambulisho wa kisheria
-Inavutia wahisani
-Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake
-Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
-Ugomvi wa mara kwa mara
-Haina kinga kwa waazilishi ukilinganisha na makampuni

Ukishachagua mfumo mzuri wa biashara yako, unatakiwa kuanza mchakato wa kuisajili katika mamlaka ya usajili wa makampuni inayoitwa BRELA, Ila yote hayo yanaweza kufanikiwa kwa msaada wa DILEX BUSINESS SOLUTION, Kupitia DILEX BUSINESS SOLUTION utafanikisha usajili wako wa kampuni, jina la biashara pia utapata ushauri bure kabisha, *Ofisi zetu zipo Block 1-Kisota-Kigamboni-Dar es salaamkaribu na kiwanda cha Tomato*


DILEX BUSINESS SOLUTION
Kama una wazo la kufanya biashara hapa Tanzania na ungependa kumiliki kampuni yako au jina la biashara lako, huduma yetu ni kufanikisha usajiri wa biashara yako. Tutumie message yenye neno “KAMPUNI” Whatsapp namnba 0716762015 kupata maelezo zaidi juu ya huduma yetu.

OFISI ZETU ZIPO
Mwalimu.J.K.Nyerere Trade Fair ground(SABA SABA), PLOT No.436, BLOCK A, Kilwa Road, Dar es salaam, Tanzania

Thanks
Contact us DILEX BUSINESS SOLUTION
FACEBOOK PAGE:Dilex Business solution
FACEBOOK PAGE:DILEX Inspire
Tell phone No: 0716762015
WHATSAPP :0716762015
E-MAIL: info@dilex.co.tz
Instagram: Dilex Business Solution

3 comments

  1. Lucas John

    Kampuni kama Facebook au Alibaba inaangukia kundi lipi hapo?

  2. Alex Limaki

    hizo ni private company

  3. Albert Makuri

    salamu Mr motinveon mm nataka kusajili kampuni kwa jina LA ÀJOMA COMPANY sasa naomba uniangalizie jina hilo kama lipo kwenye system na kama alipo niambie garama za kunisajiria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *